Nitarejea - Diamond Platnumz, Hawa

Nitarejea - Diamond Platnumz, Hawa

Год
2013
Язык
`Swahili`
Длительность
273430

Nedan finns texten till låten Nitarejea , artist - Diamond Platnumz, Hawa med översättning

Låttexten " Nitarejea "

Originaltext med översättning

Nitarejea

Diamond Platnumz, Hawa

Vipi mizigo umeshaweka tayari

Sijechelewa nkaachwa na gari

Basi jikaze usilie mpenzi

Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi

Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna

Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna

Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina

Nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka tumaa

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi

Ukumbuke na moyo utajawa na simanzi

Ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke yangu honey

Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah

Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani

Sina wakunitua nyumbani ntaliaa

Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo

Hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo

Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh

We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi

Usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki

Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki

Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi

Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ooh

Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki

Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Ntarejea mama

Niombee nirude salama

Ohhh watoto wadanganye

Ihh, ohh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

2+ miljoner sångtexter

Låtar på olika språk

Översättningar

Högkvalitativa översättningar till alla språk

Snabbsökning

Hitta texterna du behöver på några sekunder